Breaking News

BREAKING: Polisi wamaliza kupekua nyumba ya Lissu na makosa yake mawili

on

Taarifa iliyotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mchana huu imesema kwamba Jeshi la Polisi Dar es salaam limemaliza upekuzi nyumbani kwa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu.

Baada ya kumaliza upekuzi huo limemrudisha Lissu tena kwenye kituo kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa ajili ya taratibu nyingine za kisheria kuendelea, ikiwa ni pamoja na dhamana yake.

Taarifa hiyo ya CHADEMA imesema upekuzi uliofanyika ulihusu makosa mawili anayotuhumiwa nayo ambayo ni (1.) Kusema makosa ya rais hadharani  (2.) uchochezi kuhusu kushikiliwa ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 nchini Canada.

BREAKING NEWS: Magazeti yote ya Tanzania kusajiliwa upya

EXCLUSIVE: AyoTV yamtembelea Jakata Kikwete Msoga asema “nanenepa siku hizi, zamani mlikua mnanifuja”

Soma na hizi

Tupia Comments