Top Stories

Agizo la Waziri Nchemba kwa Jeshi la Polisi “msiwaachie”

on

Baada ya ajali ya Basi la City Boys na Lori iliyotokea mkoani Tabora jana na kusababisha vifo vya watu 12, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi D r Mwigulu Nchemba leo Bungeni ameagiza Jeshi la Polisi nchini kuanza kuwakamata na kuwaweka mahabusu madereva wote wanaokamatwa kwa makosa ya mwendo kasi barabarani.

“Kwakuwa imeonekana watu wamechukua kimazoea mambo ya kutoza faini baada ya kukamatwa kwa makosa ya mwendokasi barabarani, naelekeza Jeshi la Polisi popote watakapomkamata dereva anaenda mwendokasi akamatwe, apelekwe ndani na asiachiwe mpaka watakapompeleka Mahakamani ” –Waziri Nchemba

BASATA wametoa tamko tena kuhusu ROMA

Soma na hizi

Tupia Comments