Top Stories

Majonzi:Kifo kilivyomfika Malcom, alivyokimbizwa Hospital kuokoa uhai “Dakika za Mwisho”

on

Ikiwa bado tuko kwenye Simanzi na Majonzi baada ya kufariki kwa mtoto wa Mtangazaji Masoud Kipanya aitwae Malcom Ally.

Sasa hapa tumempata mtangazaji aitwae Bonge kutoka Radio Clouds FM akieleza marehemu Malcom alivyokimbizwa hospitali kuokoa Uhai.

Akizungumza na Ayo TV alisema…..”Jana mida ya saa tatu asubuhi Power Breakfast ilipoisha Masoud Kipanya aliniambia kuna safari ya kwenda hospitali nikamuuliza wapi akaniambia ni Upanga akaniambia Mama Malcom amempigia kwani hali ya Malcom si nzuri basi nikamwambia hakuna haja ya kuchukua uber basi tulipofika hospitali ya Tiba tukamkuta mtoto anatibiwa na mama yake alikuwepo pale basi tukabahati kuona ile X RAY ilivyo Daktari akasema na  X Ray haipo vizuri sana basi ngoja aanze kumtoa uchafu kinywaji kwani Malcom alikuwa hawezi hata kukohoa”-Bonge wa Power Breakfast

“Kwenye Saa sita na nusu niliondoka hospitali pale na nikaacha wote ila kwenye muda wa saa Nane Mchana nilipigiwa simu na Masoud kuniuliza kuwa niko wapi kwani alinimbia hali ya Malcom ilibadilika kwahiyo ilibidi nitoke nilipokuwa Kijitonyama mpaka Delina ambapo alipokuwa akiishi Malcom na Mama yake si mbali”- Bonge

“Basi baada ya kufika pale nilimkuta Malcom amelala kisha nikamkagua kwa kumshika mikono mara Masoud akanipigia simu kujua kama nimefika akaniuliza hali ya Malcom iko vipi nikamjibu kwamba mimi sio mzoefu ila mtoto amebadili amechoka sana”– Bonge wa Power Breakfast

MANENO YA MWISHO YA MALCOM KWA MAMA YAKE, ALIJITABIRIA KIFO, “MAMA NAKUFA TAFUTA MTOTO”

 

TAZAMA MWILI WA MALCOM ULIVYOINGIZWA KABURINI, HUZUNI ZATAWALA

Soma na hizi

Tupia Comments