Kutoka Bungeni Dodoma leo May 2, 2017, Mbunge wa Kawe Halima Mdee amepewa adhabu ya kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge la Bajeti vilivyobaki kuanzia leo. Adhabu hii imetolewa baada Mbunge huyo kutumia lugha ya matusi dhidi ya Spika Job Ndugai na Naibu Waziri wa Afya Hamis Kigwangallah.
#BREAKING Kamati ya Bunge imetoa adhabu kwa Halima Mdee MB kutohudhuria vikao vya Bunge la Bajeti vilivyobaki alitoa lugha ya matusi Bungeni pic.twitter.com/Qo6GBuk3dC
— millardayo (@millardayo) May 2, 2017
Kamati ya Bunge pia imemsamehe Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe baada ya kukiri kosa la kudharau Mamlaka ya Bunge April 4, 2017. Mbunge mwingine ni Ester Bullaya ambaye amepewa karipio baada ya kukiri kosa lake sawa na Mbowe.
Kamati ya Bunge imemsamehe Mwenyekiti wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe baada ya kukiri kutoa kauli za kudharau Bunge April 4, 2017 pic.twitter.com/ZRdW7zgEjd
— millardayo (@millardayo) May 2, 2017
Kamati ya Bunge imetoa karipio kali kwa Mbunge Ester Bulaya, baada ya kukiri kosa la kudharau Mamlaka ya Bunge alilolifanya March 30, 2017. pic.twitter.com/7zgPhKke8N
— millardayo (@millardayo) May 2, 2017
VIDEO: Tazama hapa kipindi cha maswali na majibu Bungeni leo May 2. 2017.