Michezo

Hii ndio klabu iliyomchukua Ramadhani Singano (Messi)

on

.

.

Ikiwa imepita siku moja toka  Kamati ya Haki na Hadhi za Wachezaji ya TFF kuvunja mkataba wamchezaji Ramadhani Singano (Messi)  na iliyokuwa klabu yake Simba leo hii amesaini mkataba wa kuichezea klabu ya Azam Fc .

Singano amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo inayonolewa na muingereza Stewart Hall na ataungana na kikosi hicho muda wowote kutokea hivi sasa.

.

.

Ikumbukwe kuwa wiki kadhaa zilizopita kulikuwa na utata wa ki mkataba kati ya Singano na Simba kwa zile tofauti zilizotokea ndani ya mkataba ambazo nakala ya mkataba wa mchezaji inaonyesha kumalizika mwezi june 2015 wakati ule wa klabu ukionesha june 2016.

Chanzo:Saleh Jembe blog

 

 

Tupia Comments