Matumizi ya vifaa vinavyokuwezesha kupata huduma za intaneti, ikiwa ni pamoja na simu za
kiganjani, yanatakiwa pia kuzingatia sheria na staha na pia kumhakikishia mtumiaji faragha. Mitandao ya kijamii kama vile WhatsApp, Facebook, Twitter na Instagram na mingineyo inawezeshwa kupitia intaneti.
1. Kutokuweka taarifa nyingi za binafsi na za undani kwenye mitandao ya jamii.
2. Kuwa makini kwenye matumizi ya neno la siri. Neno la siri ni muhimu sana katika kutunza anwani ya barua pepe au akaunti yako ya mtandao wa kijamii. Chagua neno la siri ambalo linachanganya maneno na tarakimu. Badilisha neno la siri mara kwa mara. Muda unaopendekezwa ni angalau kila baada ya siku 90.
3. Kutokurudia kutumia neno la siri ulilowahi kulitumia siku za nyuma. Iwapo una anwani ya
barua pepe au akaunti ya mtandao wa jamii zaidi ya moja, tumia maneno ya siri tofauti kwa kila
akaunti.
4. Ukisaidiwa kuanzisha akaunti ya mtandao wa kijamii au anwani ya baruapepe, hakikisha
unabadilisha neno la siri baada ya kukabidhiwa akaunti na anwani.
5. Kutokutoa kwa mtu yeyoye, hata wa karibu, neno la siri unalotumia kwenye anwani au
akaunti zako.
6. Usiandike mahali popote neno la siri unalotumia. Tumia maneno ambayo ni rahisi kwako wewe
kukumbuka lakini magumu kwa mtu mwingine kukisia.
7. Usijibu ujumbe mfupi unaopokea kwenye akaunti yako ya barua pepe au simu unaokutaka
kutuma taarifa zako ili zihakikiwe.
8. Usijibu ujumbe wowote wa barua pepe unaokueleza kuwa umeshinda “Bahati Nasibu”
ambayo hukushiriki kucheza.
KESI YA BIL 5.4 YA MALKIA WA TEMBO AMEKUTWA NA HATIA