Bondia mtanzania Hassan Mwakinyo aliyeibuka na ushindi ndondi baada ya kumchapa mpinzani wake raia wa Uingereza Sam Eggington katika pambano lililochezewa Birmingham, alipata mwaliko rasmi katika Bunge la Tanzania na baadae akapata nafasi ya kuzungumza na Waandishi wa Habari nje ya ukumbi wa Bunge ambapo ameelza kwa upana changamoto alizopitia hadi kufika hapo.
“Katika vitu sitavisahau ni kwamba mimi nilisafiri hapa kama mfungwa, nilikosa kibali na nikaondoka kama mkimbizi, nimeondoka mimi kwa kuazima ada ya mwanafunzi anasoma, tumekopa ada yake ya shule ili tukalipie VISA. Hii imeniuma ingawa leo kila mtu anajitokeza na kusema yeye ni meneja wangu na nasikitika kusema sina Meneja yoyote ” – Hassan Mwakinyo