Premier Bet SwahiliFlix Ad Vodacom Ad

Top Stories

Binti amuua Mwanae nae kajinyonga “Kilichofanyika ni kitendo cha kutisha” (+video0

on

Binti wa miaka 22, Ephrazia Maneno, Mkazi wa Kijiji cha Nyaseke kata ya Bulela Mjini Geita anadaiwa kumuua kwa kumnyonga Mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu kisha naye kujinyonga.

Tukio hilo limetokea Jumapili August 18, 2019 saa saba mchana umbali wa mita 300 kutoka nyumba aliyokuwa akiishi, alitumia khanga kujinyonga katika mti wa mwembe.

Maneno Kapunda, Baba mzazi wa Efrazia amedai binti yake alikua akiishi na Babu na Bibi baada ya Wazazi kutengana na hakueleza tatizo lolote kabla ya kufanya uamuzi wa kujiua

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyaseke, John Maguta amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Polisi walifika eneo la tukio na kutoa mwili uliokuwa ukining’inia na kuruhusu familia kuendelea na taratibu za mazishi yaliyofanyika Jumatatu Kijijini hapo.

RC MWANRI ‘KAAMSHE DUDE’ “TEMBEZA MKONG’OTO KICHWA KILIE KAMA NGOMA YA DAKU”

Soma na hizi

Tupia Comments