Miongoni mwa wasanii ambao walitokea kwenye mashindano ya Bongo Star Search Meninah yupo kwenye orodha hiyo na kupitia millardayo.com ameongelea project yao mpya ambayo amefanya yeye na moja ya kati ya waimbaji toka Angola Linda Ines. ‘Tumekutana hapa hapa Tanzania yeye alikuja hapa Tanzania na alikuwa akiona nyimbo zangu kwenye mitandao ya kijamii mwisho wa siku alipata namba yangu akanipigia tukaanza kuongea baadae mimi niliandika hii nyimbo nikaona hata yeye anaweza kuifanya kifupi sisi ni marafiki ambao tumekua kama ndugu na yeye hajui kabisa kiswahili anajua maneno machache kama habari na mambo’
‘Ilichukua muda kidogo mpaka yeye kurekodi huu wimbo lakini tulienda studio nikawa namuelekeza neno moja baada ya lingine nikawa namwambia Linda ingiza kinyago nipishe nimenogewa na penzi lake kuna muda anakosea si unajua mtu kama lugha ikiwa si yako kwa sababu anapenda kuimba na ana sauti ya kuimba lakini mwisho wa siku akaimaliza’
‘Kuna vitu vingine vizuri sana tunatarajia kuvifanya mimi na Linda kwa pamoja, Angola mimi kule nina nyimbo zangu tayari nimeshazituma na wanazipenda sana,Ijumaa tunategemea kuachia kazi yetu inayoitwa Kaniganda ambayo video yake itafuata baada ya wiki tatu tumeanza kuwasiliana na Director kwa sababu script tushaipitisha na tunategemea kufanya na Raymond Kasoga wa Dreamz Video’
‘kiukweli kufanya kazi na mtu asiyejua kiswahili ni kazi sana kwa sababu Linda anaongea ki-Portuguese mimi jina langu limetokea huko na likimaanisha Msichana Mrembo,nimefurahi kufanya kazi na Linda kwasababu kwanza ni muelewa na yeye pia ananielekeza lugha ya kwao,Kaniganda tumeimba kama tunamgombania mwanaume mmoja’.