Habari za Mastaa

Nicki Minaj azishambulia Tuzo za MTV VMA 2015 atoa malalamiko yake Twitter, Taylor Swift amjibu!

on

Minaj

Headlines kubwa sasa hivi kwenye industry ya muziki Marekani ni Tuzo za MTV VMA 2015 orodha yake ikiwa imetoka tayari ili watu wote waijue.

Lakini kuna baadhi ya wasanii ambao wanaonekana kutokuridhishwa na orodha hiyo, mmoja wao akiwa superstaa wa Hiphop Marekani Nicki Minaj.

minaj 2

Nicki Minaj

Licha ya kuchaguliwa kwenye category 3, Nicki Minaj aliamua kusema ya moyoni kupitia mtandao wa Twitter na kudai video ya wimbo wake wa Anaconda kutokuwepo kwenye category ya Video bora ya mwaka ni kitendo kilichomshangaza.

>>>“Kama ningekuwa msanii wa aina tofauti, Anaconda ingechaguliwa kama video bora ya mwaka pia… lakini wasanii wengine wa kike wakiachia video inayovunja rekodi na kuwavuta watu wengi wanaishia kuchaguliwa kwenye kipengele hicho…hmm!!” <<< Nicki Minaj.

tay

Taylor Swift

Design kama Nicki Minaj anatupia dongo kwa nominations 9 za Taylor Swift aliposema “wasanii wengine wa kike” akimanisha “wazungu”… Nimekusogezea baadhi ya tweets za Nicki Minaj hapa chini ili uweze kujisomea na wewe…

Na majibizano kati ya Taylor Swift na Nicki Minaj Twitter yalikuwa hivi…

NICKI 2 NICKI 4 NICKI 5 NICKI 6

Nicki Minaj anawania kipengele cha Best Female Video, Best Hip-Hop Video na Best Collaboration kwa mwaka huu.

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments