Top Stories

Mwenyekiti wa baraza la Wazee Chadema afikishwa Mahakamani

on

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CHADEMA Hashim Juma Issa (63), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka mawili ikiwemo kuchapisha taarifa za uchochezi kwa lengo la kumdhalilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro. 

Akisoma mashtaka hayo, Wakili wa Serikali Yusuph Aboud alidai Mshitakiwa huyo alitenda makosa hayo October 1 mwaka huu mtaa wa Ufipa, Kinondoni, Dar es Salaam ambapo katika shitaka la kwanza ilidaiwa akiwa eneo hilo alichapisha taarifa ya uongo kwa njia ya kompyuta na kusambaza katika mtandao wa YouTube kwa lengo la kumchafua na kumdhalilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro.

Ilidaiwa alichapisha kuwa ‘IGP Sirro ni gaidi namba moja hapa nchini Tanzania na fisadi’ na katika shitaka la pili ilidaiwa katika tarehe na eneo hilo, alichapisha taarifa ya uchochezi kwa lengo la kutengeneza chuki kwa Wananchi dhidi ya IGP Sirro kuwa ‘IGP Sirro ni gaidi namba moja hapa nchini Tanzania na fisadi’.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo upande wa mashitaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo upo katika hatua za mwisho hivyo wapangiwe tarehe nyingine ya kutajwa na Hakimu alikubali ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 28 mwaka huu huku Mshitakiwa akiachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana likiwemo kuwa na wadhamini  wawili wenye vitambulisho vya kura au cha taifa watakaosaini bondi ya Sh.Mil 3 kila mmoja.

MAJALIWA ACHUKIZWA WAMAMA KUTOKEA BARABARANI NA NDOO, AMUITA MHANDISI ‘TUAMBIE UKWELI, HAUJIAMINI’

Soma na hizi

Tupia Comments