Ni raha kuwa na Familia, mtu na mke wake wote mnafanya kazi Industry moja halafu wote mnafanya poa na watu wanakubali kazi zenu.. hiyo ni raha sana kiukweli !! Pata picha Jay Z na Beyonce wake..
Lakini moja ya Familia ya mastaa walioteka soko la muziki East Africa, Nameless na Wahu ni mfano mzuri wa mastaa ambao wamedumu kwenye Ndoa yao kwa miaka 10 na wote wanafanya muziki… “Ndoa sio kitu rahisi, mnatakiwa kusomana na kila mmoja amkubali mwenzake vile alivyo… mnatakiwa kuheshimiana pia” >>> Hii ni nukuu ya alichokisema David Mathenge aka Nameless, staa wa muziki Kenya na mume wa Wahu.
“Kuna wakati mimi na Wahu tunachokana, na najikuta nasema kwamba sikuhitaji tena na yeye anasema hivyo hivyo hataki kuniona tena…. Lakini mara nyingi tunaenda kwa washauri halafu mambo yanakuwa sawa… Tulianza uhusiano tukiwa wadogo sana wakati huo tuko Chuo… Tulipendana, tukakua pamoja.. Tumetafuta maisha pamoja na kwa sasa tuna msingi mzuri sana wa maisha yetu” >>> Nameless.
Wako mastaa ambao wanaamini wakioa au kuolewa wanajiongezea majukumu na kufanya washuke kimuziki, unaweza kucheki mfano mzuri kwa hawa watu wetu wa +254, ndoa miaka 10 na wako pazuri tu !!