Habari za Mastaa

Barua ya Tupac aliyomuandikia Madonna sasa kuuzwa rasmi

on

Inaonekana kuwa vitu vingi alivyoviacha Marehemu 2Pac vinapigwa mnada kwa sasa hii inajumuisha  barua ya rapper huyo aliyowahi kumuandikia Madonna kipindi yuko jela mwaka 1995 kwa lengo la kutaka ajue kuwa wameachana rasmi.

Inaripotiwa kuwa Mahakama mjini New York ilifuta kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamama Darlene Lutz ambaye alifunguliwa shtaka na rafiki yake Madonna mwaka 2004 kutokana na Darlene kutaka kuiuza barua hiyo na sasa inaelezwa Mahakama imetoa ruhusa ya barua hiyo kupigwa mnada, itauzwa Milioni 200 za Kitanzania chini ya kampuni ya Memorabilia company

Barua ya Tupac kwa Madonna

Inaelezwa kuwa sababu kuu ya Tupac kumuacha Madonna ni utofauti wa rangi kutokana na yeye kuwa mweusi na Madonna kuwa mwenye asili ya kizungu (Mweupe) na pengine watu wangekua wakimdharau kutokana na yeye kuwa mweusi hata kazi zake za muziki kushuka.

VIDEO: IRENE UWOYA NA BATULI WAIZUNGUMZIA SWAHILIFLIX, MTANDAO UTAKAOUZA KAZI ZAO

Soma na hizi

Tupia Comments