Ni msanii kutoka label ya PKP kwenye single ‘usiende mbali’ aliyomshirikisha Boss wake kwenye label ambaye ni Ommy Dimpoz ambayo kwa sasa inachezwa kama wimbo mkubwa kwenye TV ya Ufaransa, TRACE URBAN.
Nedy ameongea na millardayo.com na kusema ‘Kiukweli ni kitu kikubwa kwangu ambacho kimenipa faraja kubwa kwasababu kwa Tanzania ni kitu ambacho tunaweza kukizungumzia ni kikubwa kwa msanii, namshukuru Mungu wameipokea na kuiweka katika nafasi ya Smash Hit’
Nedy ni miongoni mwa Wasanii wa bongofleva utaowakuta sio waongeaji sana na pia hapendi kuona umaarufu wake unaongezeka sababu ya skendo ndio maana kataka yote yapite mbali, siku zote amekua akisema hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Shilole.
Kuna zile picha zilisambaa akiwa na Shilole lakini Nedy anasema ni rafiki tu wa kawaida, ni mshkaji kama mshkaji mwingine na kupiga picha sio ishu, ni kama anavyopiga na wengine pia.
ULIIKOSA HII YA JOKATE KUKAMILISHA HILI KWENYE SHULE YA SEKONDARI JANGWANI BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA