Habari za Mastaa

Nelly hajaoa mpaka leo, na hii ndio sababu kubwa ya yeye kubaki bachela..!

on

Msanii wa muziki wa HipHop Marekani, Nelly ameingia kwenye headlines za burudani baada ya interview aliyoifanya siku chache zilizopita kwenye moja ya radio shows kubwa New York, Marekani kuweka stori nyingi mitandaoni… je unafahamu kuwa Nelly ana watoto lakini hajaoa mpaka leo? sababu inayomsukuma yeye kuishi maisha hayo ni ipi?

Akiwa kwenye kipindi cha radio na Angie Martinez wa Radio Power 105.5 ya Marekani, Nelly alishare na mtangazaji huyo mambo mengi yanayohusu muziki wake pamoja na familia yake… na alipoulizwa kwa nini mpaka sasa hajaoa msanii huyo alikuwa na haya ya kusema…

NELLYMAR1

Nelly.

>>>Sina haraka ya kuoa japo sipingi watu kufunga ndoa… ila issue kubwa inayonisumbua mimi ni kwamba inaonekana watu wengi huharakisha kufunga ndoa lakini baada ya muda mfupi utasikia wanapeana talaka na kugawana mali…  misingi ya ndoa haijawekwa ili watu waje kufanya hivyo bali imewekwa kwa misingi mikubwa zaidi, mpaka kifo kitakapowatenganisha…

NELLYMAR3

>>> binafsi nipo radhi kuchukuwa time ya kutosha na kufanya mambo ya uhakika, kwa sababu watu wa siku hizi wana sura mbili na wanabadilika ndani ya sekunde… kwa upande wangu sina mchezo na ndoa na nikija kuoa mke wangu asitegemee kupokea talaka yoyote kutoka kwangu kwasababu naamini kuachana kwetu itakuwa mpaka pale kifo kitakapotutenganisha’…<<< Nelly.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments