Habari za Mastaa

Mama mzazi wa 21 Savage aingilia kati sakata la Mwanae kukamatwa

By

on

Baada ya sakata la rapper 21 Savage kukamatwa na Maafisa wa uhamiaji nchini Marekani siku kadhaa zilizopita kwa madai ya kuishi kiharamu nchini humo huku cheti chake cha kuzaliwa kikithibitisha kuwa amezaliwa nchini Uingereza.

Mama mzazi wa 21 Savage ameonyesha kukasirishwa na watu kufanya sakata la mwanae kama sehemu ya kutengeneza vichekesho na kuvipost kupitia mitandao yao ya kijamii. Kupitia instagram story mama 21 Savage ameeleza kuwa inaumiza kuona watu wanafanya vitendo kama hivyo.

“Ni aibu kubwa kuishi kwenye dunia ya watu wanaolishwa nguvu hasi na kucheka wenzao wanaopitia changamoto za maisha na kupigania uhuru wa maisha yao, Inaumiza lakini mwisho watu wataona tu. Hili nalo litapita Muachie huru 21 Savage” >>>Mama wa 21 Savage

Jumapili ya February 3,2019 rapper 21 Savage alikamatwa na maafisa wa uhamiaji na kudai kuwa sio raia wa nchi hiyo na kuelezwa kuwa VISA yake ya kuishi Marekani iliisha mwaka mmoja baadae alipoingia nchini humo kihalali akiwa na umri wa miaka 7.

Ulipitwa na On Air ya Historia, Wazazi wa Nandy walivyompeleka Nandy kwa Mganga?

Soma na hizi

Tupia Comments