Fahamu kuwa sanamu la Mfalme wa Pop Marehemu Michael Jackson limeondolewa kwenye makumbusho ya taifa ya mpira wa miguu nchini Uingereza wiki hii kufuatia tuhuma zinazomkabili za unyanyasaji wa kingono kwa wavulana wadogo.
Makumbusho hayo ambayo yapo kwenye mji wa Manchester yamekuwa yakiionyesha sanamu hiyo tangu mwaka 2014 lakini yameiondoa ghafla wiki hii, siku chache baada ya makala ya “Leaving Neverland” kurushwa hewani nchini humo siku ya Jumatano.
Kwenye filamu hiyo vijana wawili wanaodai kuwa wahanga wa kitendo hicho, Wade Robson na James Safechuck wamefunguka kwa undani jinsi walivyofanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kimono na Marehemu Michael Jackson kwa miaka mingi tangu walivyokuwa wadogo.
VIDEO: MWILI WA MTANGAZAJI KIBONDE ULIVYOWASILI AIRPORT DSM