Msanii kutokea Marekani, Nicki Minaj jana aliziandika headlines kwenye kurasa za burudani baada ya taarifa kusambaa kuwa amepigwa stop kwenda kutoa show Angola jumamosi ya tarehe 19 December wiki hii, kutokana na Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Angola kupinga kufanyika kwa show hiyo.
Wanaharakati hao walimuandikia Nicki Minaj barua kumuomba rapper huyo asitishe show hiyo ya Christmas iliyoandaliwa na kampuni ya simu ya Unitel, kampuni inayomilikiwa na familia ya Rais wa Angola, Rais Jose Eduardo kwa madai ya kuwa show hiyo ya Christmas imeandaliwa na fedha za rushwa hivyo haitakuwa sawa kwa yeye kukubali kutoa show hiyo!
Leo December 17 2015 stori kuhusu show ya Nicki Minaj nchini Angola ipo tofauti sana… Show ya rapper huyo itafanyika kama kawaida licha ya pingamizi hilo kutoka kwa Wanaharakati wa Haki za binadamu. Kupitia Instagram page yake, Nicki alipost picha na caption iliyosema…
>>> “ANGOLA! Mpo tayari kwa ajili ya show?!???! Can’t wait to see you guys! Nunueni ticketz zenu!” <<< @NickiMinaj
Baada ya kushare news hiyo na zaidi ya watu milion 47 wanaomfuatilia rapper huyo kwenye Instagram, Nicki Minaj akaamua kushare na watu wake wa Twitter hisia zake…
>>> “Kila neno baya litakalosema juu yangu litahukumiwa” <<< @NickiMinaj.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.