Huenda umepata taarifa zilizoenea mitandaoni kuhusiana na mtikisiko wa ndoa ya mastaa wawili kwenye industry ya muziki kutoka Kenya, Nameless na Wahu, lakini unajua Nameless kaizungumziaje taarifa hiyo?
Mwanamziki David Mathenge maarufu kama Nameless amekasirishwa na taarifa zilizoenea kwenye mitandao kuhusu kutoa talaka kwa mke wake Wahu.
Stori ni kwamba zilienea taarifa kuanzia siku ya jumamosi juu ya Nameless kuandaa talaka kwa mkewe huyo ambaye wana watoto wawili.
Nameless alikutana na stori katika mitandao ikiwa na maelezo kuwa sababu ya kuvunjika ndoa hiyo ni matokeo ya vipimo vya DNA kuonyesha kuwa Nameless sio baba halali wa mtoto wao mmoja.
Nameless na Wahu wameandika katika ukurasa wa facebook kulaani taarifa hizo hasa kwa kuvuka mipaka na kumhusisha mtoto wao.