AyoTV

Kauli ya JPM kwa Wakandarasi wabovu “Lazima tufanye maamuzi” (+video)

on

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amesema suala la Wakanadarasi katika wizara hiyo imekuwa changamoto na makosa mengi yamefanyika ambapo wanakiri wamefanya makosa kwa kuchukua wakandarasi ambao hawana uwezo.

Profesa Mbarawa ameyasema hayo wakati akikagua miradi ya DAWASA, Kimbiji Kigambano ambapo amesema hata Rais John Magufuli kwenye mkutano na viongozi wa Dini alizungumzia changamoto ya mradi wa Chalinze ambapo Mkandarasi aliopewa mradi huo amebainika hana uwezo.

“Yule mkanadarasi uwezo wake ni mdogo, hafai lakini from know where watu bila kuelewa wakamchukua na matokeo yake shida ndio zile tunapambana nazo, hivyo ili kuondokana na tatizo hilo kuna mpango tumeuweka wizarani ili kupata wakandarasi bora,”amesema.

Pia Profesa Mbarawa amewataka watendaji wa DAWASA kuhakikisha wanasonga mbele kwani wanachokitaka wananchi ni maji na sio suala jingine, hivyo lazima wasonge mbele.

MWENYEKITI UVCCM ATEMA CHECHE KWA VIJANA “TUNAKIKWAZO CHA UZOEFU”

Soma na hizi

Tupia Comments