Jana Jumatatu tarehe 07 December 2015 Tuzo za Grammy zilitangaza orodha ya wasanii waliofanikiwa kuingia kwenye nomination list ya tuzo za 58 za Grammy yani The 58th Grammy Awards huku Kendrick Lamar akiongoza list hiyo kwa kuwa kwenye vipengele 11.
Moja kati ya majina ambayo hayakuwepo kwenye list hiyo ya nominations ni jina la R&B Superstaa, Omarion. Hit single ya Omarion ‘Post To Be’ feat. Chris Brown & Jhene Aiko pia haikufanikiwa kuchaguliwa kwenye nominations hizo licha ya single hiyo kufanya vizuri sana na kupata zaidi ya watazamaji milioni 300 kwenye YouTUBE.
Staa huyo kutoka kwenye kundi la muziki la Maybach Music Group aliamua kupeleka hisia zake kwenye page yake ya Twitter ambapo alishusha hasira na masikitiko yake kwenye hizi tweet 6 nilizofanikiwa kuzinasa…
>>> “Post to be” ni moja kati ya ngoma za R&B yenye collabo kali sana. CB, Jhene & mimi mwenyewe tumekuwepo kwenye gemu zaidi ya miaka 10+” <<<
>>> “Licha ya kuwa watu wanajifanya ni kazi rahisi kutengeneza hit (& wala sio). Kama msanii unategemea kutambulika na game.” <<<
>>> “Siku zote kumekuwa na visa vinavyofanyika dhidi yangu. Na kila mara nawadhibitishia kuwa mmekosea. Mara kwa mara nimekuwa nikifanya vitu vikubwa na itawabidi mnitambue.” <<<
>>> “Hii sio “nimekasirika” (post to be). Hii ni aaha- sawa kwahiyo ile haikukithi viwango. Nitarudi. Andaaeni Grammy yangu.” <<<
>>> “Toka nitambulishwe kwenye game, game imebadilika sana. Bado wanataka wanifanye kama mimi bado ni mgeni kwenye hili. Muda wangu unakuja amini“. <<<
>>> “Kwahiyo yote yatakapo semwa na kufanyika. Kumbuka. Nilitabiri kila kitu. Hii ndio hatima yangu. Nimechaguliwa.” <<<
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.