Mix

Ugomvi wa baba na mke wake umefanya mtoto wao kupata ulemavu..

on

Fighting
Mwanaume mmoja Nigeria Udeme Inim amekamatwa kwa madai ya kumshambulia na kumng’ata sikio mtoto wake wa kiume wakati akiamulia ugomvi kati yake na mke wake nyumbani kwao mtaa wa Asaka, Nigeria.

Kulitokea ugomvi kati ya wawili hao, Inim alianza kumpiga mke wake ndipo kijana huyo Christopher Bassey alipoingilia kwa lengo na kumwokoa mama yake lakini baba yake alipatwa hasira na kumng’ata sikio na kulikata.

Father-Bits-Off-Son’s-Ear-For-Trying-To-Stop-Him-From-Beating-His-Mother

Bassey alipelekwa Hospitali ya jirani lakini madaktari hawakufanikiwa kurudishia sikio hilo, mwanaume huyo alikamatwa na kushtakiwa kwa kosa la kushambulia  na kuwekwa jela  huku dhamana yake ikiwa ni Naira 20,000 (sawa na Tshs. 180,000/-).

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments