Mix

Wanasema hizi ni picha 5 za vitu nadra ambavyo hutoviona kila siku

on

Leo February 25 nimekukusanyia picha tano ambazo wenyewe wanasema zimepigwa kwenye mazingira ya kushangaza zaidi ambapo picha ya kwanza ni hii ya samaki mwenye meno ya binadamu.

Samaki ni chakula kizuri haswa kiafya lakini ukikutana na Samaki wa aina hii kidogo lazima ushtuke na hii ni kutokana na kuwa na meno yaliyofanana na ya binadamu.

 2  Mtu akipitisha kidole kwenye Jicho lake 

Mtu huyu jina lake ni Billy Owen ambaye alilazimishwa na Madaktari kuondoa sehemu moja ya Jicho lake hali iliyomfanya kubaki na jicho moja ambapo hata hivyo Billy ameamua kuitumia hali hiyo kama sehemu ya kuwaburudisha watu na kumuonesha mtu wa tofauti.

3 Tai akijigeuza angani

Mpiga picha wa huyu Tai alichukua sifa za kutosha baada ya kuweza kumnasa Tai alivyojigeuza angani.

Ndege Flamingos katika Shape ya Flamingo

Picha hii ilipigwa na mpiga picha mtaalamu Bobby Haas kutoka huko Peninsula Yucatan, Mexico, imewaonyesha Ndege wengi aina ya Flamingo wakitengeneza Umbo lao la (Flamingo

5 Farasi aliyepaa angani akiwa kabeba Mtu

Sio rahisi kumshuhudia Farasi akiwa amepaa angani umbali huu lakini Mpiga picha wa hii alifanikiwa kumnasa na ni moja ya picha 6 za leo.

VIDEO: Huyu jamaa alikamatwa na bangi Kagera lakini alivyojitetea kila mtu alicheka, tazama kwenye hii video hapa chini

VIDEO: Tazama huyu jamaa aliyeigilizia sauti ya Mstaafu Jakaya Kikwete mpaka watu wakacheka, bonyeza play hapa chini…

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments