Bado headlines za anayetajwa kuwa kocha ghali kwa sasa duniani Pep Guardiola anakwenda kufundisha klabu gani zinazidi kuchukua nafasi, tayari Pep Guardiola ametaja nchi atakayokwenda kufundisha soka baada ya kukiri kuwa hatoendelea na kuifundisha klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani.
Pep Guardiola amekiri kuamua kuondoka ndani ya klabu ya FC Bayern, baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mitatu, sababu zinazomfanya Guardiola aondoke klabu ya FC Bayern ni kuwa yeye bado kijana na anahitaji changamoto mpya katika maisha yake ya ukocha.
Lakini Guardiola kathibitisha kuwa asingependa kuustafu ukocha bila kufundisha klabu za Uingereza, hivyo kwa kauli hiyo tayari Guardiola anakuwa katoa uhakika wa kwenda Uingereza ila klabu bado haipo wazi atakayojiunga nayo ” Nafikiri mimi bado kijana, ndio kwanza nina umri wa miaka 44, nahitaji changamoto mpya na nisingependa kustaafu bila kufundisha soka Uingereza” >>> Guardiola
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE