Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga amefanya ziara ya ghafla leo Dec 16 2015 katika makambi mbalimbali ya Jeshi la Polisi Dar es salaam na kutoa amri kwa viongozi wa jeshi hilo siku mbili za kuhakikisha amepata taarifa kuhusu udhibiti wa dawa za kulevya.
“Wapo wajanja wana mbinu nyingi, lakini hawawezi kutuua. Na mimi hili ni jambo nitalivalia njuga, lakini kwanini katika ukamataji wa dawa za kulevya sisi tulioko kwenye operesheni tunakaa pembeni? Nataka jibu siku ya Ijumaa”
Kuhusu watu kubambikiziwa kesi, Waziri limemgusa na kalizungumzia pia “Hili la kubambika watu kesi tunaweza kuliondoa hata leo, kikubwa ni kuwa na nidhamu, inakuwaje unambambika mtu kesi ili akuletee pesa? Hiki ni kitendo cha rushwa na tuliangalie kwa pamoja na tutaliongea kwa undani Ijumaa”
Hapa nimekusogezea pia baadhi ya picha za Waziri Kitwanga katika ziara yake.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana naMillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE