Ishu ya mastaa wa kibongo kukopi nyimbo za nje imesikika sana, ambacho tumezoea kukiona kwa kawaida ni kwamba wenzetu kama Marekani wanafuata sana Sheria, ukiangalia Chris Brown aliimba ‘she ain’t you’ kwa kuiga wimbo wa Marehemu Michael Jackson– ‘Human Nature’, lakini kuna utaratibu ambao ulifuatwa wa masuala ya hakimiliki mpaka Chris akapata ruhusa kurudia wimbo huo.
Hii ni moja ya story chache kuwahi kuzisikia tena eti imetokea Marekani, Pharell Williams, Robin Thicke na rapper T.I kuhusishwa na tuhuma za kukopi idea ya wimbo wa Marehemu Marvin Gaye.
Watoto wa Marvin wamefungua mashtaka Mahakamani kwamba Pharell na wenzake wamekopi wimbo wa baba yao unaoitwa ‘Got to Give It Up’ katika wimbo wa ‘Blurred Lines’ ambao ulifanywa na Pharell, Robin na T.I.
Pharell amesema hajakopi wimbo huo lakini wakati akiuandika kulikuwa na hisia kichwani kwake za nyimbo hizo mbili kufanana lakini hiyo haimaanishi kwamba amekopi idea au mashairi ya wimbo huo.
Kesi inaendelea ambapo rapper T.I. ataitwa Mahakamani pia kwa ajili ya kutoa ushahidi wake.
Kaa karibu yangu kupitia Facebook Twitter na Instagram kwa kubonyeza hapa na nitakusogezea kila kinachonifikia mtu wangu >>> Facebook Twitter Instagram