Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ametuma pongezi zakw kwa Rais mteule wa Malawi Dr. Lazarus Chakwera kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo.
“Nakupongeza Dkt. Lazarus Chakwera kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Malawi, kwa niaba ya Serikali na Watanzania wote naahidi kuendeleza uhusiano wetu wa kidugu, kirafiki na ujirani mwema hususani katika masuala ya uchumi na ustawi wa jamii, Hongera sana Rais” Rais Magufuli