Michezo

RC Paul Makonda ateuliwa Simba SC

on

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam RC Paul Makonda leo ametangazwa rasmi na Simba SC kuwa ameteuliwa kuwa mshauri mkuu wa bodi ya wakurugenzi wa Simba SC, taarifa hizo zimetolewa kupitia ukurasa rasmi wa instagram wa Simba SC.

Makonda anatangazwa nafasi hiyo ikiwa ni siku chache zimepita toka MO Dewji atangaze nia yake ya awali ya kujiuzulu nafasi ya mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi lakini RC Makonda akatumia ukurasa wake wa instagram kuwatuliza mashabiki wa Simba SC kuwa haamini kama hayo ni maamuzi ya MO Dewji,

Siku iliyofuatia MO Dewji akafuta uamuzi wa kujiuzulu, inadaiwa kuwa RC Makonda ni miongoni mwa watu waliomshauri MO Dewji kufuta uamuzi huo kwa maslahi mapama ya Simba, Paul Makonda amekuwa shabiki wa Simba SC kwa muda mrefu ambaye hasiti kuonesha mapenzi yake hadharani.

AUDIO: DR Kigwangalla ahoji bilioni 4 za MO Dewji Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments