AyoTV

VIDEO: Makamu wa Rais Samia alivyozindua utoaji wa ‘IPAD’ kwa wanafunzi Dodoma

on

March 13 2017 Makamu Wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alizindua mpango wa Ugawaji wa Vishikwambi “IPAD” 5, 000, Laptops na Projectors kwa Shule za Msingi 10 za Jimbo la Dodoma Mjini.

Makamu Wa Rais amesisitiza kuhusu utunzaji wa vifaa hivyo na matumizi sahihi ya vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kusaidia kuinua kiwango cha Elimu katika Jombo la Dodoma Mjini

Aidha Makamu wa Rais amepongeza jitihada na ubunifu wa Mbunge la Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde na kuahidi kuendelea kumpa ushirikiano katika kuwahudumia wanadodoma Mjini.

Samia amewataka wasimamizi watakaokabidhiwa misaada hiyo wahakikishe wanaitunza na wale watakaoshindwa watatakiwa kujiwajibisha wenyewe kabla ya kuwajibishwa

Full video nimekuwekea hapa chini…

VIDEO: Maamuzi ya Dr. Tulia baada ya kukuta ubovu kwenye shule aliyosoma Mbeya 

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments