Habari za Mastaa

Najua hautopenda kupitwa na hizi picha nyingine alizonitumia Ay akifanya video yake na Sean Kingston Marekani

on

Ay 3Mabibi na Mabwana…… kwa mara nyingine tena Ay ambaye ni msanii wa Tanzania amerudi kwenye headlines za kuruka kimataifa baada ya zile ahadi kutimia za kufanya single pamoja na staa wa dunia Sean Kingston.

Niliwahi kumsikia akiongea zaidi ya mara nne kwamba kolabo hii ingefanyika lakini haikuwa hivyo kutokana na sababu ambazo zilizokuwa nje ya mipaka yake ambapo bila kukata tamaa, Ay ameweza kuvumilia kwa miaka yote hii toka alipoahidiwa na Sean aliekuja Tanzania mwaka 2010.
Ay 1Ay alishawahi kuipa nafasi millardayo.com kusikiliza single aliyoifanya na Sean Kingston zaidi ya mwaka mmoja na nusu uliopita lakini alichelewa kuitoa sababu hakutaka kuitoa bila video hivyo baada ya ratiba za Sean kukaa vizuri ndio wameingia mzigoni.

Ay 2

Ay 4Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments