Habari za Mastaa

Mastaa 6 wa Marekani wenye umri usiofanana na mwonekano wao

on

Waswahili wanasema “Umri ni namba” wakikusudia unaweza kuwa na miaka mingi lakini wajihi wako ukakutambulisha kama mwenye umri wa kati na wapo watu mbalimbali hasa maarufu ambao mara zote unazoweza kumuona huwa katika muonekano ule ule licha ya umri wake kusogea.

Sasa leo September 2, 2017 ninayo list ya mastaa sita ambao wana umri mkubwa lakini muonekano wao hauoneshi kama umri umeenda.

1. Pharrell Williams

Ni mwimbaji wa miondoko ya Pop, mwandishi wa nyimbo na producer. Ana umri wa miaka 44 lakini anaonekana tofauti kabisa na ulivyo umri wake. Picha hii ina tofauti ya miaka 11.

Image result for pharrell picture difference then and now

2. Gwen Stefani

Ifikapo October 3 Mwanamuziki Gwen atakuwa anatimiza umri wa miaka 48, ana mume na watoto watatu. Katika picha hii hapa chini ni tofauti ya miaka 12.

Image result for then and now pictures of gwen stefani

3. Sandra Bullock

Ni mwigizaji na mtayarishaji wa filamu wa Marekani ambaye ana umri wa miaka 53. Ana mume na watoto wawili lakini katika picha hii ni tofauti ya miaka 13.

Image result for then and now pictures of Sandra Bullock

4. Jennifer Lopez

Mwimbaji, muigizaji, mwanamitindo ambaye amekuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mastaa kibao akiwemo P Did. Ana umri wa miaka 48 na katika picha hii ni tofauti ya miaka 14.

Image result for then and now pictures of Jennifer Lopez

5. Julia Roberts

Inga wa picha hizi zina tofauti ya miaka 20 lakini mwigizaji Julia Roberts ambaye October 28 atatimiza miaka 50 lakini haonekani kuzeeka na bado anaendelea kuwa mrembo kila siku.

Image result for then and now pictures of Julia Roberts

6. Will Smith

Mwanamuziki na Mwigizaji ambaye amekuwa na mafanikio zaidi kwenye uigizaji kuliko muziki. Baadaye mwezi huu, September 25 atakuwa na umri wake ni miaka 49 lakini haonekani kufanana na umri huo. Picha hii ina tofauti ya miaka 21

Image result for then and now pictures of Will Smith

Uliiona hii? Joh Makini aongelea Kiki za bongo, views ndogo Youtube na mengine

VIDEO: Dogo Janja alivyomkimbia P FUNK baada ya kuona msg za mapenzi alizomtumia mwanae Paula, UTACHEKA ANAVYOSIMULIA….. bonyeza play hapa chini kumtazama

 

Soma na hizi

Tupia Comments