Bilionea wa kitanzania Saniniu Laizer ambaye alipata madini ya Tanzanite kwa nyakati tofauti amekamilisha ujenzi wa shule yake aliyoijenga nakuipa jina la Saniniu Laizer ambapo ujenzi wake umetumia million 466.
Shule hiyo imezinduliwa na katibu tawala wa wilaya ya Simanjiro Zuena Omary ambapo amesema itapewa vibali haraka nakuahidi kushirikiana naye ikiwa ni pamoja nakupeleka waalimu.