Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Mtuhumiwa wa kwanza wa mauaji ya Nispey akutwa na makosa mengine

on

Inaripotiwa kuwa Mahakama mjini Los Angeles imewapokea mashahidi wawili ambao wanadai kuwa mtuhumiwa wa kwanza wa mauaji ya Nipsey Hussle, Erick Holder’29 alimtishia bastola na kumpiga nayo jamaa mmoja kabla ya kufanya tukio la mauaji ya Nipsey Hussle siku ya March 31,2019.

Kwa mujibu wa mtandao wa Complex unaripoti kuwa kisa cha Eric Holder kufanya tukio hilo ni kuwa alitoa malalamiko kuwa kijana huyo alimuuzia bangi iliyochanganywa na madawa mengine na hivyo kuchukua maamuzi ya kufyatua risasi.

Hata hivyo Eric Holder alikamatwa April 3,2019 na kufikishwa mahakamani na alisomewa mashataka yanayomkabili April April 4,2019 lakini taarifa za awali zilidai kuwa polisi walimlipa mtuhumiwa Eric Holder kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 170 za Kitanzania ili kufanya mauaji hayo

VIDEO: NANDY AONYESHA STUDIO YAKE ALIYOJENGA NYUMBANI, KAONGELEA SHOW YA SUMBAWANGA NA MTOTO WA RUGE

Soma na hizi

Tupia Comments