Michezo

TFF wamfungia Luc Eymael na faini

on

Kamati ya maadili ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) leo imetangaza kumuadhibu aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga SC raia wa Ubelgiji Luc Eymael kwa kumfungia miaka miwili kufanya kazi za soka nchini.

Pamoja na adhabu hiyo aliyopewa Luc Eymael amepigwa faini ya Tsh milioni 8 kutokana na makosa yake aliyoyafanya ya kutoa kauli zilizotafsiriwa kuwa za kibaguzi na kufanya Yanga SC kumfuta kzi mara moja.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Luc Eymael alitoa kauli za kibaguzi siku ya mchezo wa mwisho wa Yanga wa Ligi Kuu dhidi ya Lipuli FC mkoani Iringa.

Hata hivyo Luc Eymael amekuwa ni kocha anayeingia katika migogoro ya mara kwa mara na waajili wake kwani Kenya katika klabu ya AFC Leopards aliondolewa kwa aibu na kufungiwa mlango.

Afrika Kusini pia kupitia chama chao cha soka SAFA wameiunga mkono Yanga SC na TFF kwa kumuadhibu Luc Eymael kutofanya kazi nchini kwao kwa kosa alilofanya Tanzania la ubaguzi wa rangi.

Soma na hizi

Tupia Comments