AyoTV

VIDEO: Ally Choki kaondoka Twanga Pepeta? kataja alipo sasa

on

Msanii mkongwe wa muziki wa Dance nchini, Ally Choki amerudi kwenye headlines baada ya kutangaza April 8, 2018  kuwa ameondoka rasmi kwenye bendi yake ya zamani Twanga Pepeta baada ya mkataba kuisha.

Nguli huyo wa muziki wa Dance aliyasema hayo baada ya kukutana na waandishi wa habari kwenye usiku wa uzinduzi wa saloon ya kisasa Respect Barber Shop iliyokutanisha mastaa mbalimbali.

‘Hapa tunazindua saloon lakini ningependa kuwaambia mashabiki wangu kwangu kuanzia sasa hivi napatikana pale The Mafik Band napiga show pale nextdoor kila Jumapili, mimi niko rasmi The Mafik Ally Choki

Mkataba wangu Twanga Pepeta ulimalizika tangu April 1 mwaka huu na sasa hivi kurudi itakuwa ngumu kwasababu nimesharudi mara nyingi, mimi ni mwanamziki nina uwezo mkubwa kufanya kazi’- Ally Choki

Unaweza ukabonyeza play kutazama alichokizungumza Ally Choki

Soma na hizi

Tupia Comments