Kupitia mtandao wa The Blast unaripoti kuwa Rapper French Montana anadaiwa kodi ya kiasi cha zaidi shilingi Million 900 za Kitanzania kutokana na kudaiwa kodi tokea mwaka 2016 kiasi hicho cha fedha kitazidi kuongezeka mpaka malipo yatakapokamilika.
Inaripotiwa kuwa Mamlaka ya kodi mjini California imetoa muda kwa Rapper huyo kukamilisha deni linalomkabili haraka iwezekanavyo kinyume na hapo mamlaka hiyo italazimika kuchukua vitu vyake vyote vya ndani na kuvipiga mnada.
French Montana alipata mafanikio makubwa kwenye ngoma ya ‘All the way Up’ mwaka 2016 na pia anatajwa katika mafanikio ya kundi la Ghetto Kids kutokea Uganda baada ya kuwajengea nyumba pamoja na kuchangia ujenzi wa kituo cha afya nchini humo.
SHILOLE KAFUNGUKA “Wolper aolewe sasa, nimeamia kwangu madili mengi”