Mix

Soudy Brown yupo na Jaguar…ishu ni yule kijana aliyeruka ukuta wa Ikulu ya Kenya…#Uheard (Audio)

on

jaguar

Siku moja baada ya kijana wa Kenya Mathew Maina kusimamishwa mahakamani kwa kuruka ukuta wa ikulu bila hofu alijitetea anataka kuonana na rahisi ili apewe ela ya kurekodi studio kutokana na kukosa pesa.

Baadhi ya wasanii Kenya wameingilia kesi hiyo na kuingia kwenye mgogoro na mahakama pamoja na Serikali wakati kijana huyo akiwa bado mahakamani huku siku ya jana mahakama ikiomba apelekwe kwanza hospitali kupimwa akili kabla ya kushtakiwa

Jaguar ambaye ni mmoja wa wasanii wakubwa Kenya ameingilia mzozo huo na kupinga kijana huyo kushtakiwa, amesema haoni kosa la kijana huyo kwani ameonyesha ujasiri kutaka kupata msaada na ametamani kama angeenda kwake ili aweze kumsaidia afanye vyema katika muziki wake.

Isikilize hapa mtu wangu…

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments