Mix

Jokate kayajibu haya kuhusu uhusiano wake na Ali Kiba walivyokutwa pamoja Nairobi Kenya… #UhearD (Audio)

on

kiba

Tetesi za uhusiano kati ya Jokate na Ali Kiba zimeendelea kubeba headlines nyingi kwenye mitandao ya kijamii lakini wenyewe mara nyingi wamekuwa wakikataa kuhusu stori hiyo, kuna ukweli wowote?

Ali Kiba na Jokate wameonekana pamoja tena Nairobi Kenya, akapewa nafasi Mrembo Jokate kuzungumzia kwa mara nyingine kuhusu kile kinachosemwa wao kuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Jokate amesema wanapeana sana support kimuziki, hakuna kingine chochote kinachoendelea kati yao.

Kingine Jokate amemsifu sana Ali kwamba jamaa sio mtu wa maneno mengi ndio maana amekuwa karibu naye, na kingine kizuri kwa Ali ni moyo wake… Kidoti anasema hata stori za Kiba kuhusishwa na beef hajui zinatokea wapi !!

Hapa anaanza Soudy Brown kuielezea U Heard yenyewe alafu yuko pia presenter wa XXL, B Dozen ambaye alikuwa Nairobi Kenya na ndio aliyepiga stori zote na Jokate na kumsogezea Gossip Cop 88.4 Dar es Salaam.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments