Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Ukaribu wa Country Boy & Young Lunya ‘buku ndio ilituunganisha’

on

Imekuwa ngumu kwa Wasanii wengi nchini kufunguka kuhusu mahusiano yao ya kimapenzi, leo February 8,2019 Rapper Countryboy amefunguka mengi alipokuwa kwenye mahojiano na kipindi cha XXL cha Clouds FM ikiwemo ishu nzima ya mahusiano yake.

” Nipo kwenye mahusiano na najua watu wengi hawakunizoea kuniona nikiweka wazi mahusiano yangu, Mtu ambaye nipo nae alikuja kwenye maisha yangu kipindi ambacho sikuwa sawa lakini alionyesha upendo na ana nafasi kubwa sana kwangu kwani ni mshauri mzuri na anapenda ninachokifanya na hata muda huu ananisikiliza ili kuhakikisha kama kweli nimefika hapa kwenye XXL”

” Mimi na Young Lunya ni washkaji wa kitambo na nakumbuka tulikutana mwaka 2012 kwenye kumbi ya starehe na yeye alikuwa amepoteza buku na sisi ndiyo tuliyoiokota na kuanzia hapo ukaribu ukaanza, Tunakuja na ngoma yetu mimi Babuu pamoja na Lunya”

DUUH! MREMBO KATOKA KIJIJINI KAPELEKWA GUEST KAAMKA KADEKI GUEST NZIMA ?

Soma na hizi

Tupia Comments