Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Miaka 22 ya Kifo cha Rapper 2Pac Shakur

on

Leo September 13,2018 ni kumbukumbu ya kifo cha nguli kwenye muziki wa Hip Hop Rapper 2Pac Shakur ambaye alizaliwa June 16,1971 na kufariki September 13,1996  baada ya siku kadhaa kupita baada ya kupigwa risasi akiwa anaendesha gari mjini Las Vegas Marekani.

Jina lake la kuzaliwa ni Tupac Amaru Shakur ila wengi wanamfahamu kwa jina la 2Pac au Makaveli, enzi za uhai wake aliwahi kuingia kwenye Guinness World Record kutokana na mauzo ya album yake kutajwa kufikia milioni 74 Dunia nzima lakini milioni 44 kwa mauzo ya Marekani pekee kama msanii wa muziki wa Hip Hop.

Marehemu 2Pac alitamba na ngoma nyingi kali zikiwemo Hit Em Up, Dear Mama, Only God Can Judge Me, Life Goes On na nyingine nyingi aliwahi pia kushiriki kwenye filamu mbalimbali ikiwemo Poetic Justice akiwa na Janet Jackson , Above the Rim, Juice.

Alikiba kamwambia Ommy Dimpoz “usiwaze Mungu kakunusuru wote si wake”

Soma na hizi

Tupia Comments