Top Stories

Walimu wote nchini Uganda kuchanja lazima

on

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema Shule zitaendelea kufungwa nchini humo hadi January, 2022 ikiwa ni juhudi za kudhibiti Corona na ni lazima Walimu na Wafanyakazi wote Mashuleni wawe wamechanjwa kabla ya kufungua Shule.

“Vyuo vya kati na Vyuo Vikuu vitafunguliwa November 01,2021 lakini kwa pia Walimu na Wafanyakazi wengine wa kawaida wote wawe wamechanjwa”

“Hadi kufikia leo kati ya Walimu walengwa 550,000 ni Walimu 269,945 pekee ndio ambao tayari wamechanja dozi ya kwanza na Walimu 96,653 ndio wamepata dozi zote mbili, hii inafanya Walimu 280,055 kuwa bado hawajachanja, hatuwezi kufungua Shule wakati bado hawajachanja”- Rais Museveni

“MWENDOKASI MBAGALA UJENZI UNASUASUA , MKANDARASI ASIMAMIWE, ASISINGIZIE MGOMO” — RC MAKALLA

MAMA AANGUA KILIO, TUKIO LA MWANAE KUUAWA KWA MAPANGA, PICHA NA VIDEO ZINAZOSAMBAA MTANDAONI

Soma na hizi

Tupia Comments