AyoTV

Jackline Wolper kahojiwa na Zamaradi na kuyaongea ya mapenzi yake na Harmonize

on

Ni kwenye Exclusive Interview ya TAKE ONE ya CloudsTV ambayo inasimamiwa na Zamaradi Mketema na ishu kubwa aliyoiongelea ni uhusiano wake wa kimapenzi uliopita na wa sasa ambao yuko na mwimbaji wa bongofleva Harmonize ambaye yuko kwenye lebo ya Diamond WCB.

Kwenye Interview hii ndefu moja ya maneno aliyoyasema Wolper ni haya >>> ‘Rajabu (Harmonize) sijamjua hivi karibuni nimemjua siku nyingi sana nilikua namchukulia kama Mwanamuziki tu, kuja kugundua kwamba Rajabu alikua ananikubali siku nyingi tukawa marafiki, alikuja kunitamkia kwamba ananipenda nikiwa kwenye wakati mgumu sana na mtu niliyekua nae

Tuna mwezi mmoja na wiki mbili sasa hivi toka tumeanza kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi, sitaki kuigiza kwenye swala la mapenzi…. nilikua na mtu ambaye nilikua naamini atakua mume wangu na pete na kidole nilimpa lakini haikutokea, swala la familia na Rajabu linakuja

Mimi kuwa na Harmonize sio maigizo ni kitu kiko serious, najua kuna watu wengine wanasema Harmonize huyo Chokoraa sijui ameimba nyimbo mbili, sasa kama nimeweza kuwa na mtu wa aina yangu alafu amenitenda alafu unakuja kuniambia mtu ana nyimbo mbili eti nisimpende, mimi sihitaji pesa… naweza kuwa hata na mwendesha bodaboda nikambadilisha‘ – Wolper

Ukitaka kuipata full Interview ya Wolper na Zamaradi Mketema bonyeza play hapa chini..

ULIKOSA KUONA ILIVYOKUWA KWA HARMONIZE NA WOLPER KWENYE BIRTHDAY PARTY? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI..

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments