Staa wa muziki kutoka Nigeria Yemi Alade ni mmoja wa wasanii kutoka Africa wanaohesabika kuwa na ushawishi mkubwa kwenye soko la muziki la Africa… Nimekutana na interview moja ya Yemi Alade aliyofanya siku chache zilizopita, ndani yake staa huyo amegusia vitu vitatu vikubwa; safari yake ya muziki, sababu iliyopelekea single ya Johnny kuandikwa na mafanikio aliyoyapata kupitia single hiyo.
Haya ndiyo aliyoyagusia Yemi Alade kupitia interview yake na Not Just Ok Tv…
Safari yake kimuziki ilianzaje: “Kwanza sikuwahi kuwaza kama ningeweza kutengeneza biashara ya kusimama na muziki, sikujua kama ningeweza… lakini baada ya kushinda shindano la kusaka vipaji mwaka 2010 niligundua kuwa inabidi nitengeneze kitu kupitia kipaji changu na mara ya kwanza naingia studio ilikuwa kazi ngumu sana kurekodi (sikuzoea haraka) licha ya kuwa kipaji changu ni zawadi kutoka kwa Mungu…“
Ilikuaje mpaka akaitunga single ya Johnny: “Nilikuwa nafanya media tour ya single yangu mpya Nigeria… badaaye mtu akaniuliza kwa nini wasanii wa kike wa Nigeria wanaimba nyimbo lakini hatuwasikii wakiwataja wakaka ndani ya single zao… nikawaza nikaona sawa ngoja nijaribu kufanya hivyo, nikakutana na Selebobo ambaye tulirekodi wote single ya ‘Johnny’… na ule wimbo tuliurekodi tukicheka sana maana mistari yake ilikuwa inafurahisha!“
Mafanikio aliyoyapata kupitia single ya Johnny?: “Kwanza sikuwahi kuwaza Johnny itakuja kuwa single kubwa kama ilivyo leo… wimbo wa Johnny umegusa watu wengi sana na umaarufu wa wimbo huo unanizidi hadi mimi, pia bado unaendelea kusumbua chati nyingi duniani na kwa sasa video ya Johnny imepata watazamaji zaidi ya watu milion 27 YouTUBE na pia ni video ya msanii wa kike wa Africa iliyotazamwa zaidi YouTUBE… Mafanikio yapo mengi sana ila hayo ni baadhi tu!“
Bonyeza play kuitazama video ya Johnny hapa chini:
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.