Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

VIDEO: Arnold Schwarzenegger kapigwa teke na shabiki Afrika Kusini

on

Muigizaji wa filamu maarufu na Gavana wa California, Marekani Arnold Schwarzenegger alijikuta akipigwa teke la mgongo na kijana mmoja nchini Afrika Kusini alipokwenda kwa ajili ya kuhudhuria tamasha la michezo liitwalo ‘Arnold Classic Africa’ jijini Johannesburg siku ya  Jumamosi May 18,2019.

Staa huyo ambaye amepata umaarufu kupitia filamu nyingi nchini Marekani alikuwa akirekodi matukio kwenye mtandao wa snapchat yake,  baada ya kumaliza alishangaa akirukiwa mgongoni na kupigwa teke  na baadae ikaelezwa kuwa kijana huyo alidhibitiwa na walinzi waliokuwepo maeneo yale.

Kwa mujibu wa mtandao wa Twitter Schwarzenegger aliandika kuwa alifahamu kuwa alihisi ni mashabiki wamemsukuma kwa bahati mbaya hadi kuanguka ila baada ya kuliona tukio hilo kwenye video ndio akagundua kuwa alikuwa ni shabiki tu, Schwarzenegger  anafurahi kuwa hakuharibu video yake aliyokuwa anairekodi kwa ajili ya Snapchat account yake.

VIDEO: SHAMSA FORD AJITANGAZA KUWA SINGLE “MA-SINGLE LADIES TUAKATAFUTE HELA”

Soma na hizi

Tupia Comments