Zoezi la uokoaji bado linaendelea hapa Nyamkazi, Bukoba ilikopata ajali Ndege ya Precision leo asubuhi ambapo Vikosi vya uokoaji na Watu mbalimbali wameendelea kuongeza jitihada ili kuitoa Ndege hiyo ndani ya ziwa.
Baada ya zoezi la kuivuta Ndege kwa kamba kuonekana kutofanikisha uokoaji kama ilivyotarajiwa, waya na kamba ngumu zimeongezwa kwenye eneo la tukio pamoja na magari maalum ya kunyanyulia/kuvuta vitu vizito ili kurahisisha uvutaji huo, @AyoTV_ na millardayo.com zipo hapa kukuletea updates zote.