Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Zuchu alamba dili Spotify
Share
Notification Show More
Latest News
Basata wafika kwenye msiba wa H Mbizo Morogoro, ‘Mazishi ni Dar’
January 28, 2023
The After Party ya Marioo kufanyika Elements Bar Masaki DSM Usiku wa leo
January 28, 2023
Picha: Katibu Mkuu wa CCM amewasili Wilayani Gairo Mkoani Morogoro
January 28, 2023
Uamuzi wa Baraza la Mashekhe Mkoa kuhusu Ndoa ya Dr Mwaka na Queen Masanja
January 28, 2023
Ukatili wa Wanafunzi shuleni, “Maafisa Elimu wapewa rungu”, washughulikieni Walimu
January 28, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Habari za Mastaa > Zuchu alamba dili Spotify
Habari za Mastaa

Zuchu alamba dili Spotify

May 6, 2022
Share
3 Min Read
SHARE

Msanii wa Afropop na Bongo Flava kutoka Tanzania Zuchu ndiye balozi mpya kwa mwezi wa Mei, wa program ya muziki iitwayo “EQUAL Africa” kinacho endeshwa na Spotify. Lengo la programu ya “EQUAL” ni kuimarisha usawa wa kijinsia katika muziki kwa kuwaonyesha wanawake wa Ki-Afrika wenye vipaji wanaotikisa mawimbi katika tasnia hiyo na kutoa jukwaa la kuwaenzi.

Tangu kuzinduliwa kwake katika siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani mwaka 2020, Spotify imekua ikiendesha programu ya EQUAL kila mwezi ambapo wasanii wa kike mbalimbali huangaziwa kutokana na vipaji na umahiri wao katika tasnia ya muziki. Kila mwezi, msanii wa kike huchaguliwa kuwa Msanii wa EQUAL na mojawapo ya nyimbo zake kutumika kama kichwa cha nyimbo za EQUAL Africa.

Baadhi ya wasanii ambao wameangaziwa hadi sasa ni pamoja na Tiwa Savage wa Nigeria, Fave, Ayra Starr na Asa; DBN Gogo wa Afrika Kusini na Nomfundo Moh; na Gyakie na Amaarae wa Ghana. Vilevile, Zuchu anaungana na nyota wa Afrika Mashariki Muthoni Drummer Queen, Malkia wa Kenya na Silvia Sssaru katika kukuza sauti za wanawake wa Kiafrika wenye vipaji kupitia EQUAL.

Akiwa mzaliwa wa familia ya kimuziki na kwa sasa akiwa amesajiliwa na rekodi ya Diamond Platnumz ya WCB, Zuhura Othman Soud (almaarufu kama Zuchu) ni mtoto wa mwanamuziki nguli wa Taarab, Khadija Kopa, ambaye aliimba naye wimbo wa “Mauzauza.”

Zuchu aliingia kwenye ulingo wa muziki kwa mara ya kwanza mwaka 2015 kupitia shindano la kutafuta vipaji lenye mada ya karaoke mjini Lagos, Nigeria. Kisha mwimbo wake maarufu wa “Cheche” aliomshirikisha Diamond Platnumz ukamzulia umaarufu mnamo 2020. Mwaka uliofuata, alitoa wimbo uliovunja rekodi, “Sukari,” ambao umepata wasikilizaji zaidi ya milioni 2 wa Spotify.

“Mbali na kunionyesha uwezo wa kimuziki unaoweza kutoka kwa uzoefu wa wanawake katika muziki, program hii pia imenisaidia kutambua kwamba tunaweza kushinda vikwazo ambavyo ni sehemu ya kufanya kazi katika ulimwengu unaotawaliwa na wanaume wa Afrobeats, ” asema Zuchu akiwakumbuka wanamuziki wote wa kike ambao wamemtia moyo katika safari yake.

“Kuwa sehemu ya programu ya “EQUAL”, ni jambo kubwa kwangu na inasaidia kuhimiza wanamuziki wengine wa kike kuvumilia na kuvunja vizuizi vya jinsia katika nyanja ya muziki,” anaongeza.

Wimbo mmoja wa Zuchu “Mwambieni“, uliotolewa mapema mwaka huu, umeangaziwa kwenye orodha za kucheza za EQUAL Africa na EQUAL Global kwenye Spotify.

“Tunafuraha kubwa kwa Zuchu kajiunga na program ya EQUAL. Ni dhahiri kuwa ni mmoja wa wasanii wenye vipaji vingi kutoka Tanzania, na hii ni sifa anayostahili,” anasema Phiona Okumu, mkuu wa muziki wa Spotify Kusini mwa Jangwa la Sahara akiongeza kuwa Spotify imejitolea kuwaangazia wasanii wa kike barani Afrika kwa matumaini kwamba mpango huu utawahamasisha wasanii wengine wachanga na wajao katika tasnia ya muziki kudumu kwenye njia sahihi na kuendelea kufanya kile wanachofanya.

You Might Also Like

PROFILE: Mfahamu Vido Vidox, ripota wa Ayo TV kwa stori za mastaa!!

Exclusive: Dully Vanny kwa uchungu azungumzia video chafu aliyotajwa, amtaja diamond na mama yake

Audiomack yazindua kampeni ya ‘Ngoma juu ya ngoma’ kukuza muziki wa kitanzania

Exclusive: Con boi kafunguka hana mawasiliano na Lunya,Quick Rocka, akumbuka kifo cha mpenzi wake

Mkali Burna boy ametuletea hii video mpya akiwa amemshirikisha Ed Sheeran

TAGGED: habari za mastaa
Pascal Mwakyoma TZA May 6, 2022
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo May 6, 2022
Next Article Lisha ya Tems kushirikishwa kwenye collabo ya Drake na Future ila hajaonekana katika video
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Basata wafika kwenye msiba wa H Mbizo Morogoro, ‘Mazishi ni Dar’
Entertainment January 28, 2023
The After Party ya Marioo kufanyika Elements Bar Masaki DSM Usiku wa leo
Entertainment January 28, 2023
Picha: Katibu Mkuu wa CCM amewasili Wilayani Gairo Mkoani Morogoro
Top Stories January 28, 2023
Uamuzi wa Baraza la Mashekhe Mkoa kuhusu Ndoa ya Dr Mwaka na Queen Masanja
Top Stories January 28, 2023

You Might also Like

Top Stories

Picha: Katibu Mkuu wa CCM amewasili Wilayani Gairo Mkoani Morogoro

January 28, 2023
Top Stories

Ukatili wa Wanafunzi shuleni, “Maafisa Elimu wapewa rungu”, washughulikieni Walimu

January 28, 2023
Top Stories

Tazama Shaka alivyokula kiapo cha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa “Sitotoa siri”

January 27, 2023
Top Stories

Mapya ndoa ya Dr Mwaka haijavunjwa, tamko kali latolewa na baraza la Ulamaa

January 27, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?