Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Baada ya Kajala kuiona video inayosambaa na wanaosema ni mtoto wake

on

Kwa siku za hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii kumekua na video inayosambaa inayomuonyesha binti mdogo akifanya mapenzi ndani ya gari huku taarifa za kwenye mitandao hiyo ya kijamii zinadai kuwa binti huyo ni mtoto wa muigizaji Kajala Masanja ambaye anaitwa Paula.

Kajala ameona hiyo taarifa na kupitia akaunti yake ya Instagram ameamua kuandika >>’Hey everyone….jamani mimi sina shida na mtu kama akinichukia au akinisema mimi kwa kitu chochote kile…kwasababu najua binadamu kuongea mmezoea ila katika kuongea kwenu kuingilia na kujudge maisha yangu naomba msimuingize mtoto wangu’

‘Sijawahi kumuomba mtu anisaidie kulea hata siku moja…mimi nimeona kuna video insambaa mnasema ni mwanangu na mnajua kabisa sie Paula huyo ila ilimradi tu mfurahishe roho zenu’ – Kajala

‘Nilinyamaza…ila sasa naona mnakoelekea ni pabaya..mnahisi yeye hana moyo? au haumii? mwanangu anasoma na sitaki mumchanganye na mambo yenu ya kipuuzi… vitu vibaya mnavyo muombea mwanangu viwarudie wenyewe…leave my daughter alone jamani’

…give us a break..fanyeni tu mambo yenu yatakayofanya mpate faida katika maisha yenu na sio mwanangu….na pia mjue kua mnamdhalilisha huyo binti na sio Paula tena…na huyo binti ana wazazi na familia pia…hope tumeelewana‘ – Kajala

ULIPITWA? Wema Sepetu alimwambia Zamaradi Mketema kwanini hatomsamehe Kajala, bonyeza play hapa chini kutazama

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement