PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Habari za Mastaa

Mahakama yaitupilia mbali kesi iliyokuwa ikimkabili Cardi B na Offset

on

Inaripotiwa kuwa Mahakama imelitupilia mbali shauri la mlinzi wa Rapper Cardi B na Offset kumshambulia mpiga picha mmoja mjini New York kwenye onesho la Met Gala mwaka jana 2018.

Mamlaka ya Polisi imeuambia mtandao wa TMZ kuwa mlinzi huyo hatochukuliwa hatua zozote za kisheria na shauri hilo limefungwa. Inaripotiwa kuwa Cardi B pamoja na Offset waliingizwa kwenye kesi hiyo kwa kushtakiwa kumtuma mlinzi huyo.

Inaripotiwa kuwa shabiki mmoja anayefahamika kwa jina la Daniel Szalkiewicz amefungua mashtaka na kudai kuwa alipata majereha usoni, shingoni na mgongoni katika shambulio hilo lilitokea Met Gala.

VIDEO: MC PILIPILI “SIKUWAI KUPATA MZURI KAMA HUYU, NIMEZOEA KUZINGULIWA SITAKI TENA MAHUSIANO? NI SHETANI”

Soma na hizi

Tupia Comments