Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Alichosema T.I.D baada ya kutoka nyumbani kwa Paul Makonda leo

on

Leo February 11 2017 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alimualika nyumbani kwake Masaki mwimbaji maarufu wa Bongofleva T.I.D ambaye siku 3 zilizopita aliachiwa kwa dhamana baada ya kulazwa Polisi kwa tuhuma za utumiaji wa dawa za kulevya.

Leo Paul Makonda alipomuita T.I.D nyumbani kwake walizungumza mambo mengi  na baadae mkuu huyo wa mkoa akaandika “Mungu wetu hajalala na siku zote anampenda amtafutae, karibu tena nyumbani T I D”

Sasa na T.I.D nae ameamua kuandika yafuatayo baada ya kukutana na Paul Makonda ambapo aliyaambatanisha maneno hayo na picha waliyokaa pamoja >>> “Muziki bila Madawa ya kulevya inawezekana…This is the turning Point kwangu mimi na kizazi cha mziki huu wa kizazi kipya”

Akamalizia kwa kuandika “Nikiwa na Mh. Makonda leo tukijadili jinsi gani ya kuokoa Vipaji na Sanaa kwa ujumla, Mungu ibariki Bongo Fleva,Mungu Ibariki Tanzania

VIDEO: Walivyofikishwa Mahakamani T.I.D, Rachel, Petitman na wengine, tazama kwenye hii video hapa chini

VIDEO: Wema Sepetu, T.I.D na wengine walivyoingia Polisi baada ya kutajwa orodha ya Paul Makonda 

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako Millard Ayo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID NA IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement