Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Philip Mpango ambaye ameleza Bunge kuwa Serikali haijafanya zuio kwa shirika la Fedha Duniani (IMF) kuchapisha ripoti yake kuhusu hali ya kiuchumi Tanzania kama inavyoelezwa na baadhi ya watu na kwamba kilichotokea ni Serikali inaendelea kufanya mazungumzo ya kawaida na shirika hilo kabla ya kuchapishwa kwa ripoti hiyo.
Waziri Mpango ameeleza kuwa ni suala la kawaida na taratibu za IMF kuwasilisha rasimu Serikalini kwa maoni kabla ya kuchapisha ambapo Serikali husika inakuwa na siku 14 za kujadili na kutoa maoni yake na kwamba bado mazungumzo yanaendelea.
MAAGIZO YA SERIKALI KWA ASKARI WANAOSIMAMISHA MAGARI KWA KUJIFICHA